ZABURI 127:3-5

Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.

MATHAYO 18:4

Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

MITHALI 22:6

Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

KUMBUKUMBU LA TORATI 11:19

Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo

MATHAYO 18:10

Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

Saturday, November 18, 2017

3 MINUTES DECEMBER PRAYERS

Zaidi ya wamama 7500 kwa mwaka wanapoteza uhai wao wakati wa kujifungua, sawa na zaidi ya wamama 22 kwa siku, just imagine wamama hawa wote unawafahamu na unakaa nao mtaa mmoja, inamaana mtaani kwako kutakuwa na misiba 22,   ni simanzi na huzuni isiyoelezeka, nakubali Tanzania tunachangamoto ya wahudumu wa afya wa kutosha, wakati mwingine wamama wajawazito wanaohitaji Huduma ni wengi ukilinganisha na uwezo wao wa kutoa Huduma, wakunga kuna wakati wanachoka, wanafanya kwa juhudi sana lakini ukubwa wa kazi/ kuhudumia wamama wajawazito wajifungue salama unakuwa ni mkubwa sana.
      Tunayaelekeza maombi yetu kwa wakunga wote wa Tanzania, Mungu awape nguvu ya ziada, uvumilivu, tumaini ili waokoe wamama wajawazito pamoja na watoto wao wengi kwa kadiri inavyowezekana ili kuturejeshea TUMAINI la maisha kwa wamama na watoto wao pamoja na tumaini la UPENDO kwa wamama na watoto.

Happyday, Happy Year, Happy lifetime
mr. Kids

HDM 3MINUTES DECEMBER PRAYERS to bring HOPE to life and love