Wednesday, February 10, 2016
WATOTO NI MALI YA BWANA
Marko 10:14 Ila Yesu alipoona alichukizwa
sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa
maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.
Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo
Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.