Zaidi ya wamama 7500 kwa mwaka wanapoteza uhai wao wakati wa kujifungua, sawa na zaidi ya wamama 22 kwa siku, just imagine wamama hawa wote unawafahamu na unakaa nao mtaa mmoja, inamaana mtaani kwako kutakuwa na misiba 22, ni simanzi na huzuni isiyoelezeka, nakubali Tanzania tunachangamoto ya wahudumu wa afya wa kutosha, wakati mwingine wamama wajawazito wanaohitaji Huduma ni wengi ukilinganisha na uwezo wao wa kutoa Huduma, wakunga kuna wakati wanachoka, wanafanya kwa juhudi sana lakini ukubwa wa kazi/ kuhudumia wamama wajawazito wajifungue salama unakuwa ni mkubwa sana.
Tunayaelekeza maombi yetu kwa wakunga wote wa Tanzania, Mungu awape nguvu ya ziada, uvumilivu, tumaini ili waokoe wamama wajawazito pamoja na watoto wao wengi kwa kadiri inavyowezekana ili kuturejeshea TUMAINI la maisha kwa wamama na watoto wao pamoja na tumaini la UPENDO kwa wamama na watoto.
Happyday, Happy Year, Happy lifetime
mr. Kids
HDM 3MINUTES DECEMBER PRAYERS to bring HOPE to life and love